KOFFI ANNAN
Alizaliwa
Aprili 8,1938 huko Kumasi nchini GHANA .Alizaliwa katika familia maarufu na
baba yake alikuwa ni Chifu wa kabila la Fante na akiwa kama mtumishi mkubwa
katika serikali. Annan alibahatika kupata nafasi ya kusoma akijushughulisha na
masuala ya sayansi na teknolojia nchini Ghana.Mwaka 1959 alipata nafasi ya
kwenda kusoma Nchini Marekani katika chuo cha Macalaster huko S.Paul Minnesota.
Mwaka 1961 alipata shahada yake ya kwanza katika masuala ya uchumi huko
Macalaster. Baadaye alienda kusoma Geneva,Uswisi na kupata shahada nyingine ya
Masuala ya uchumi .
Alipata kazi yake
ya Kwanza jumuiya Ya Madola katika Shirika la Chakula Duniani (WHO), Aliacha
kazi UN na kufanya kazi katika kampuni ya maendeleo ya utalii nchini Ghana
ambapo alifanya kazi hapo kuanzia 1974 hadi 1976. Miaka minne baadae . baadaye
aliteuliwa tena na UN kama Naibu Kiongozi mkuu wa shirika la wakimbizi ambapo
alifanya kazi mpaka ilivyofika mwaka 1983 alipoteuliwa kuwa mkuu wa idara ya
fedha. Mwaka 1990 kofi annan alipandishwa
cheo na kuwa assistant katika upangaji w bajeti na matumizi ya UN.ilivyofika
mwaka 1993 liteuliwa kuwa kionhozi mkuu wa mazungumzo ya amani wa Umoja wa
Mataifa.
Kofi annan ni
mwafrika wa kwanza kuwa katibu mkuu wa kwanza wa jumuiya ya madola (UN)
akiichukua nafasi hiyo Januari 1997 mpaka Disemba 31,mwaka 2001. Annan
alisifika sana kimataif na katika jumuiya ya madola akwa uwezo wake mkubwa wa
usuluhishi wa migogoro ya amani akiwa
kama Katibu Mkuu wa jumuiya ya madola. Umashuhuri wake na uwezo aliokuwa nao
ulimsaida katika nchi kama Rwanda,Somalia na hoko Yugoslavia.
No comments:
Post a Comment