JIFUNZE KISWAHILI
__________________________________________________________________
I.
USHAIRI
Kuna
mitazamo ya aina mbili katika kuelezea dhana ya ushairi. kuna wanamapokeo na
mamboleo. Hata hivyo kabla ya kuendelea zaidi kuwachambua tuangalie wataalam
mbalimbali wanavyofasili dhana hii . Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu
mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama
ifuatavyo:
MAPOKEO
Mssamba,
(2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina
inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina
ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.”
Mnyampala
(1970) anasema
kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora
sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata
iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.”
Amri
Abeid (1954:1) anasema
kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana.” 2
Abdulatifu anasema kwamba
ushairi ni ule ulio na sifa ya ulinganifu wa vina na mizani, lugha laini (lugha
tamu) na lugha hii iweze kugusa moja kama ilivyokusudiwa.
Encyclopedia
American (EA) inaeleza
kuwa ushairi ni kauli zenye hisia na ubunifu, mpangilio fulani wenye urari,
uwasilishaji wa tajiriba au mawazo ya mtunzi kwa maana ambayo huibua tajiriba
kama hiyo katika nyayo za wasomaji au wasikilizaji na kutumia lugha ya picha
yenye wizani wa sauti.
MAMBOLEO
Kezilahabi
( )anasema
kuwa “ushairi ni tukio hai au wazo ambalo limeonywa kwetu kutokana na upangaji
uzuri wa maneno fasaha yenye mizani Fulani ili kuonyesha ukweli”
Topan
(1996) anasema
kuwa “shairi ni unaoeleza hisia za ndani za binadamu kwa mpangilio Fulani wa
maneno” hivyo kwa mujibu wa Topan ushairi lazima uguse hisia za ndani ya moyo
wa binadamu.
Njogu
na Chimerah (1999) wanasema
“ ushairi ni sanaa ya lugha inayoeleza jambo kwa njia ya mkato na kwa namna
inavyoteka hisia za msomaji au msikilizaji”
Mulokozi
na Kahigi (1982:25) wanasema
ushairi ni “sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum na fasaha na wenye
muwala, kwa lugha ya picha, sitiari au ishara katika usemi, maandishi au
mahadhi ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisia
fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.”
Hivyo
basi tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa yenye kuandikwa au kuimbwa
kwa kufuata kanuni za ushairi au 3
kutofuata kanuni za ushairi ikiwa na
maana kuwa ushairi waweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo
uwe na ujumbe.
Katika
ushairi FANI na MAUDHUI ni muhimu sana, mawazo fikra au sihi za ndani ni vitu
muhimu sana katika ushairi
CHANZO/CHIMBUKO
LA USHAIRI
Dhana
ya chimbuko inafasiliwa na TUKI (2004) kuwa ni mwazo au asili ya kitu.
Baadhi
ya wataalamu wameweza kuelezea chimbuko la ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia
mitazamo au nadharia mbili ambazo ni kama ifuatavyo:
1. Nadharia ya kwanza inadai kuwa;
Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu.
2.
Na nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la
jamii ya waswahili wenyewe.
Hapa
tunaenda kuzielezea nadharia hizi kila moja na kujaribu kuona ubora wake na
udhaifu wake katika kuelezea chimbuko la ushairi
1.Na
nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii
ya waswahili wenyewe.
Kwa
kuanza na Lyndon (1962) “Swahili Poetry” anatoa hoja tatu ambazo ni:
ushairi wa Kiswahili umetokana na Uislamu,
ushairi ulianzia kwenye upwa wa kaskazini mwa Kenya hususani Lamu.
4
Na maudhui ya ushairi wa Kiswahili yalitokana na ushairi wa Kiarabu. Utungo wa
kwanza wa ushairi andishi wa Kiswahili ni Tambuka, Mwengo bin Athmani (1728)
Ubora
wa Nadharia hii
Ubora wa nadharia hii au mtazamo wa Harries kuhusu chimbuko la ushairi wa
Kiswahili ni kwamba umesaidia wengine kuendelea kuchunguza zaidi kuhusu
chimbuko la ushairi wa Kiswahili.
Udhaifu
wa nadharia hii
Udhaifu wa nadharia hii ni kuwa si kweli kwamba ushairi wa Kiswahili uliletwa
na Uislamu bali ulikuwepo hata kabla ya ujio wa Uislamu, kwani ushairi
hautenganishwi na jamii husika. Hivyo jamii za waswahili walitumia Nyanja mbalimbali
za ushairi katika shughuli zao mbalimbali au shughuli zao za kila siku, kama
vile; shughuli za kilimo na ufugaji.
Pia ushairi wa Kiswahili ulianza karne ya 10BK na ushairi wa Kiswahili ulikuwa
ukitungwa na kughanwa kwa ghibu bila kuandikwa. Wataalam wengi wanakubaliana
kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo.
Udhaifu
mwingine katika mtazamo wake wa kusema kuwa ushairi ulianzia pwani ya kaskazini
ya Kenya si kweli kwa kuwa waswahili walikuwepo hata sehemu nyingine kama vile
Kilwa na Bagamoyo ambapo ushairi wa Kiswahili ulitumika. 5
Hoja
ya kusema ushairi wa Kiswahili ulitokana na Kiarabu haina mashiko kwa kuwa
waswahili walikuwepo hata kabla ya waarabu na walikuwa na ushairi wao isipokuwa
ujio wao ulileta athari kubwa kwa kuwa ulichanganya na mambo ya dini ya
kiislamu na hati.
Knappert
(1979) “Four centuries of Swahili verse” anasema; “Ushairi wa
Kiswahili ulichipuka kwenye upwa wa Kenya kutokana na nyimbo na ngoma za
waswahili na ulianza katika karne ya 17 na pia ni ushairi wa Kiislamu wenye
kuchanganya sifa za tungo za kiafrika na za kiajemi.
Ubora
wa hoja hii ni kwamba, ni kweli Knappert amekubali kuwa,ushairi wa Kiswahili
ulitokana na waswahili wenyewe.
Hata
hivyo hoja yake ina udhaifu kwa kuwa ushairi wa Kiswahili ulianza kabla ya
karne ya 10 BK na pia amejikita katika maudhui ya mambo mengine kama vile
siasa, uchumi na kijamii. Vilevile amechanganya chimbuko la ushairi wa
Kiswahili na Uarabu.
2.
Nadharia ya pili inasema kuwa ushairi ni zao la waswahili wenyewe.
Nadharia
hii imejadiliwa na wataalam mbalimbali akiwemo Shaban Robert, Jumanne Mayoka
(1993) na Senkoro, Mulokozi na Sengo.
Jumanne,
M. Mayoka (1993) anasema
ushairi umetokana na jamii ya wanadamu wenyewe na umesheheneza ukwasi mkubwa wa
lugha ambayo imekuwa ikitumika katika hatua zote za kisiasa, kiuchumi na
kiutamaduni katika historia ambayo mwanadamu amepitia, Kwa mfano kuwa msamiati
uliotumika tangu enzi za kuishi mapangoni, enzi za uwindaji, ujima, 6
utumwa, vita vya makabila, uvamizi wa
wageni, ukoloni na harakati za kupambana na ukoloni hadi kupata uhuru na maendeleo
yake.
Ubora
wa hoja
Ubora
wa hoja hii ni kwamba ina mashiko ndani yake kwa sababu, kila jamii ina sanaa
yake na ushairi ni moja kati ya sanaa hizo ingawa inaweza ikaathiriwa na sanaa
ya jamii nyingine. Pia ushairi umekuwa ukikua na kuendelea kadri jamii
inavyokuwa na kuendelea.
Udhaifu
wa hoja.
Udhaifu
wa hoja hii ni kwamba si kweli kuwa katika kipindi hicho ushairi ulikuwa tayari
umesheheni ukwasi mkubwa wa lugha, na kama ulikuwa kweli umesheheni huu ukwasi
wa lugha alipaswa kutuonesha huo utajiri wa lugha anaouzungumzia katika
ushairi.
Senkoro
(1988) anasema
kuwa ushairi uliibuka pale lugha ilipoanza katika kipindi cha uhayawani
(kipindi ambacho mwanadamu alipoanza kupambana na mazingira yake) kwenda katika
kipindi cha urazini (maana) ili kumwezesha binadamu na mazingira yake kwa
mfano, zana za kazi zilizotumika ziliwafanya waimbe kwa kufuata mdundo wa zana
hizo.
Masamba
anasema
kwamba kimsingi chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni waswahili wenyewe katika
nyimbo, ngoma nk ambazo ziliimbwa katika masuala ya kilimo, jando na unyago
n.k. Massamba anaendelea kusema kwamba nyimbo hizi zilikuwa zikiimbwa bila
kufuata vina na mizani lakini kwa kadri muda ulivyoenda walizidi kuziendeleza
na kuziboresha. Hivyo 7
suala la vina na mizani lililetwa na
wageni sio kiini cha ushairi wa kiswahili
Mulokozi
fasili
ya fasihi haiwezi kutenganishwa na utamaduni wa maisha ya watu. Anaelezea kuwa
ushairi wa Kiswahili hutumia lugha ya Kiswahili, hivyo ili kujua chimbuko la
ushairi wa Kiswahili ni lazima ujue juu ya waswahili wenyewe
Pamoja
na kuwa nadharia hii imeonesha kukubalika na wataalamu mbalimbali kama vile
Senkoro, Mayoka na Shekhe Amri Abeid, lakini bado ina mapungufu. Hii ni kwa
sababu imeshindwa kuonesha muda maalumu ambapo ushairi wa Kiswahili ulianza na
ni wapi ulianza kutumika. Hili ni suala ambalo linaumiza vichwa vya wataalamu
mbalimbali hadi hivi sasa, kwani hakuna mtaalamu yoyote aliyefanikiwa kuonesha
ni wapi na ni lini ushairi wa Kiswahili ulianza.
Hivyo
basi, kutokana na nadharia hizo mbili tunaungana na nadharia inayosema kuwa,
chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la waswahili wenyewe, kwa sababu
waswahili wana utamaduni wao ambao ulikuwepo kabla ya ujio wa Waarabu. Na
waliutumia ushairi huo katika shughuli mbalimbali za kijamii, kwa mfano katika
harusi, jando na unyago.
AINA
ZA USHAIRI/BAHARI ZA USHAIRI
Kwa
ujumla ushairi upo katika makundi mbalimbali. Uainishaji wa ushairi unategemea
wataalam. Mlokozi (1996) anadai kuna bahari 13 za ushairi ambazo kwa
mujibu wa tapo la wataalamu wa Mombassa
1.
Wimbo/Tathilitha
8
Shairi la aina ya wimbo lina mishororo 3 inayoweza kuwa na mikondo tofauti,
unaweza kuwa na kina kimoja mwishoni
Mara nyingi wimbo huwa na vipande viwili
2.
Shairi/Tarbia
Utungo ambao una mishororo 4 katika kila beti na kila mshororo una vipande 2
Shairi huweza kuwa na maudhui ya namna yoyote ile
3.
Utenzi/utendi
Ni ushairi wenye mizani michache kuliko 12
Una vina vinavyobadilikabadilika isipokuwa cha mwisho
Kwa kawaida husimulia visa virefu vya kihistoria.mfn vita nk
4.
Zivindo
Ni shairi linalofafanua maana ya maneno
Lengo kuu ni kufunza lugha. Mfn shairi la Kihindi.
5.
Tumbuizo
Hauna idadi kamili ya mizani na mishororo
Nia yake ni kutoa hisia ambazo zimembana mtu. Mfn Mbolezi-nyimbo za misibani,
nyimbo za kubembelezea watoto
6.
Hamziyya
Una mishororo miwili miwili na vina vyake viko mwisho tu wa beti
Ulitungwa na Sharif Aidarus bin Uthman
Ulikuwa ni wa kumsifu mtume Mohamadi S.W.A
7.
Dura Mandhuma au Inkishafi
Unatokana na utenzi wa mtu aliyeitwa Inkishafi
Una mambo ya kuonya, kufuata mambo ya kidini na kuelekeza
9
8. Ukawafi
Una mstari mmoja wenye vipande vitatu
Ukwapi-silabi
6
Utao-silabi
4
Mwandamizi
5
Zinahusu maudhui ya kidini
9.
Wajiwaji
Ni utungo ambao una mishororo 5 kila ubeti wenye mizani 5
Zinahusiana na mambo ya kidini, kumsifu mtu shujaa na bingwa
10.
Wawe au Vave
Asili yake ni kaskazini ya mwambao wa Pwani hasa sehemu za Amu na Pate
Unahusu kilimo, ziliimbwa wakati wa kufyeka mistu, kuchoma pori nk
11.
Kimai
Ni utungo unaohusu mambo ya baharini au wakati wavuvi wanapomtafuta mwenzao ambaye
amepotea
Ni utungo unaohusu ubaharia
Idadi ya mizani hubadilika badilika na vina si vya lazima
12.
Ngonjera
ni mazungumzo au mabishano ya kishairi kuhusu mada Fulani
huundwa kwa kulumbana pande mbili
suluhisho la kile kinachojadiliwa hupatikana mwishoni
13.
Kikwamba
Ni utungo ambao neno moja hutumiwa kila mwanzo wa ubeti na neno hilo
hufululizwa na mabadiliko mbalimbali.
10
MABADILIKO NA MAENDELEO YA
USHAIRI WA KISWAHILI
MAENDELEO
YA KIHISTORIA:
ü Wataalamu ambao wanajaribu kutupa
taarifa kuhusu maendeleo ya ushairi wa Kiswahili ni pamoja na M.M. Mulokozi
(1996) ambaye anatuambia kwamba ulianza karne ya 10BK
ü Katika kipindi hiki hakukuwa na ushairi
ambao ulikuwa umeandikwa kwa utamaduni wa Waswahili bali kulikuwa na ushairi
simulizi uliganwa kwa ghibu
ü Kuanzia miaka ya 1000BK wakati wa
ukoloni kulitokea athari kubwa katika ushairi wa Kiswahili k.v hati ya
maandishi na dini ya kiislamu
ü Ushari uliwaunganisha Waswahili na duni
pana ya umma na taaluma ya uandishi kwa hati ya Kiarabu uliwapa wenyeji ujuzi
wa kusoma na tabia ya kuandika
1000-1500BK
ü Katika kipindi hiki kulikuwa na ustawi
na ustaarabu wa kimji wa waswahili katika miji yote ya Pwani na biashara
ilistawi kati ya wageni na wenyeji
ü Katika kipindi hiki fasihi pia ilistawi
ü Mashujaa wanaosimuliwa katika tendi k.v
Fumo Lyongo waliishi kipindi hiki
ü Ushairi uliendelea kuwa simulizi
ü Ushairi wa mwanzo uliitwa SWIFA
1500-1750BK
11
ü Hiki ni kipindi cha tatu na kilikuwa
kipindi cha misukosuko ya wenyeji na Wareno
ü Kulikuwa na tungo zilizohidhiwa
zilizowahusu Wareno, Migeni, Poatugei afila
ü Tungo nyingine zilikuwa ni utendi wa
Hamziyya, Siri Lasinari, Utendi wa Tambuka 1723 nyingi zilikuwa zikiwapa moyo
Waswahili
ü Waswahili walifanikiwa kuwaondoa wareno.
1750-1900
ü Hiki kilikuwa ni kipindi cha nne, na
kilikuwa ni kipindi cha utawala wa Waarabu
ü Kulikuwa na migogoro mingi ya kivita
katika utawala wa Waarabu
ü Tabia za Mamwinyi, wafanya biashara,
matajiri na wamisionari vilistawi
ü Kipindi hiki kilitawaliwa na fasihi ya
kidini ambayo ilitafakari theologia na falsafa ya maisha
ü Kulikuwa na tendi nyingi zilizoibuka
kuko Arabuni wakati wa mtume Muhamed. Mfn Shutaki, Angamia, Nakaa, Masahibu nk
ü Pia kulikuwa na tungo za kitamaduni,
mawaidha na tumbuizo. Mfn utendi wa Mwanakupona
ü Washairi walijitokeza kuhusu mashairi ya
kisiasa ambao ni Myaka bin Haji (1776-1840), huyu aliishi Mombassa.
KARNE
YA ISHIRINI (20) 12
ü Katika kipindi hiki uchapishaji wa
magazeti na vitabu ulijitokeza. Kulikuwa na Asasi za kudai uhuru. Waandishi
waliandika sana kuhusu kudai uhuru. Mfn Saada Kandoro
ü Baada ya uhuru ushairi wa kisiasa
ulienea zaidi kama vile Ngonjera na makue.
MAJARIBIO
NA MABADILIKO KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI
Senko
( ) anasema baada ya fahamu zake kufunguliwa alianza kuangalia mabadiliko
katika ushairi.alidai kuwa kuwa kuwa dunia inabadilika hivyo na ushairi hauna
budi kubadilika.
ü Wangai Mwai (2008:73) fasihi hubadilika
badilika katika kumbo na maudhui kwa hiyo ushairi wa Kiswahili sharti uruhusu
mabadiliko yanapotokea.
MGOGORO
WA USHAIRI WA KISWAHILI
ü Baadhi ya washairi kama vile
E.Kezilahabi, M.M Mulokozi, K.K Kahigi na wengineo walinza kuandika kazi za
ushairi zisizo na urari wa vina na mizani
ü Wengi walichukulia na kurudi nyuma kwa
ushairi lakini waandishi hao waliona ni hatua ya maendeleo
ü Hivyo mashairi yaliyotungwa kwa mfumo
huo yalipata majina mbalimbali kama vile Makue, Mtiririko, Mapingiti. Nk
ü Na hivyo watungaji wa mashairi haya
waliwaita wanamapinduzi na wengine wakawaita wachochezi
ü Ibrahim Noor Shariff (1988:183) amedai kuwa
mzozo uliibuka pale wanamabadiliko walipodai mambo matatu:
1)
Mbinu za kutunga mashairi zilikuwa chache mno
13
2) Sharia za kutunga mashairi
ziliwanyima uhuru wa kutunga
3) Muundo wa tungo za kishairi uliokuwa
wa Kiswahili hapo awali haukuwa na vina wala mizani, hivyo sharia si za lazima.
ü Kauli hizi za wanamabadiliko zilipingwa
sana na wanamapokeo ambao waliamini kwamba urari wa vina na mizani ndiyo roho
ya ushairi, ruwaza ya vina na mizani ndizo zinazoufanya ushairi wa Kiswahili
ujitambulishe.
Njogu
na Chimerah (1999:113) wanadai kwamba mgogoro huu ulikuwa baina ya vijana na
wazee waliokuwa wamekulia katika mazingira ya tungo za vina na mizani
Mawazo
yao kwa ujumla yalipingana kwa kiasi kikubwa na mawazo ya wanamapokeo japo kuna
mazingira Fulani walifanana. Wanamabadiliko waliamini kuwa
v Hakuna sheria za kutunga mashairi
(Kezilahabi 1977:60), kila shairi lina njia yake ya kutunga na njia yake ya
kutoa mawazo.
v Dhamira/maudhui, mawazo, maadili na
falsafa zitawale fani ya ushairi
v Walidai kuwa mabadiliko ya umbo la
ushairi yamefungamana na maendeleo ya historia ya jamii zetu, ni sehemu ya
jamii yetu,hivyo kubadilika kwa ushairi wa Kiswahili si kitu cha kigeni
v Vina na mizani ni kunga za utungaji
zilizozuia ushairi wa Kiswahili kukua na kusambaa kwa mapana yake na marefu
yake.
Soma
Njogu na Chimerah (1999) ufundishaji wa fasihi. 14
II.
RIWAYA
Riwaya
sio utanzu wa muda mrefu sana bali ni utanzu ambao umeanza kushika mashiko hivi
karibuni kuanzia karne ya 19 huko Ulaya
Encloypedia
hudai
kuwa riwaya ni ubunilizi ya kinathari1 inayotosha kuwa kitabu (kitabu kwa
mujibu wa UNESCO ni chapisho lolote lenye kuanzia kurasa 48 na kuendelea.)
bunilizi ya kifasihi ni ambapo matukio mengi yamebuniwa
1 nadhari-ni maelezo ya kina
yanayoelezea jambo kwa mapana (hii inafanya itofautiane na ushairi na
tamthiliya
2 Tajiriba ni uzoefu alio nao mtu. Uwe mbaya au mzuri
Enclopedia
Bratanica wanasema
“riwaya ni masimulizi marefu ya kubuni ya kinathari yaliyochangamana kiasi na
yenye kuzungumzia tajiriba2 ya binadamu. Wanaendelea kusema kwamba kwa kawaida
riwaya huwa na mfululizo wa matukio yanahusiana na yenye kulihusu kundi Fulani
la watu kaka manthari mahususi
Mphahlele
(1976) anasema
kwamba riwaya fupi huwa na kati ya maneno thelathini na tano elfu (35,000) na
hamsini elfu (50,000) na riwaya ndefu zaidi inaweza kuwa na maneno zaidi ya
sabini na tano elfu (75,000)
Mhando
na Balsidya wanadai
kwamba katika riwaya lazima kuwe na mchanganyiko wa matukio na ujenzi wa
wahusika naye Foaster (1949) anachangia kwa kusema kwamba riwaya lazima
iwe na wakati.
SIFA
ZA RIWAYA
v Ni masimulizi ya kubuni
v Ni hadithi ya nathari katika masimulizi
15
v Ni ya mpangilio au hakuna mpangilio
v Inafungamana na wakati (yaani yale
yanayotendeka katika jamii hiyo)
v Ina sifa ya urefu kama tulivyoona hapo
juu
v Ina mawanda mapana (yaani inaweza
kuzungumzia mambo kwa upana sana)
v Lazima kuwe na mchangamano wa visa
mfano; katika riwaya ya Janga Sugu la Wazawa ina visa kama, ushirikina, vifo,
mapenzi ya kweli na ya uongo,ndoa, mila nk
v Ina wahusika wengi
CHIMBUKO
LA RIWAYA
Riwaya
imejazwa na mambo makubwa mawili:
1) Fani za kijadi za fasihi
2)
Mazingira ya kijamii
a) Ngano-hadithi za kubuni zinazohusu
wanyama, watunzi wengi wameathiriwa na ngano kw wasababu wanachota visa, mbinu
za kifani , dhamira katika ngano (zinaonekana kwamba ni za kingano zaidi)
b) Visasili-masimulizi ya kubuni ambayo
yanaeleza juu ya maisha, asili, ya vitu na hatima yake. Kwa kawaida visasili
huaminiwa kuwa ni hadithi za kweli
c)
Visakale-ni hadithi za kale zinazohusu kabila la kale, udini nk. M.M.Mulokozi
anasema kuwa kila kabila lina visakale vyake. Katika riwaya visakale
vinajitokeza katika riwaya ya Kisima cha Giningi
16
d)
Hekaya-ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabu yasiyo ya
kawaida, mara nyingi masaibu yanasababishwa na mapenzi, huwa ni ndefu kuliko
hadithi nyingine lakini si ndefu kuliko riwaya. Katika taaluma ya Kiswahili ni
riwaya ya Adili na Nduguze-Shaaban Robert, Riwaya ya Ubeberu Umeshindwa
ya KIIMBILA( 1971)
e)
Tendi-ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria na wakubuni wa jamii
au taifa.mfano Utendi wa Fumo Lyongo, kuna baadhi ya riwaya zimeiga
mbinu za kiutendi. Mfano huko Ulaya Illiad Odyssey, Don Tuliv 1928, Toistoi
(1828-1910). Mfano katika Afrika ni riwaya ya Ngugi wa Thiong’o ya Matigali.
f)
Masimulizi ya wasafiri-ilihusu masaibu waliyopata wasafiri mbalimbali. Mfano
Riwaya ya kiingereza ya kwanza ni Robinson Kruso ilihusu habari ya mhusika mkuu
ambaye alikuwamo katika merikebu iliyozama na akaokoka na kuamua kuiishi katika
kisiwa peke yake. Katika Kiswahili kuna riwaya kama vile “utumwa” “Kwa
Heri Iselamagazi” hizi zote ziko katika muundo huu.
Katika
karne ya 16 fani nyingi ziliendelea. Na mojawapo ya sababu ya kuendelea kwa
riwaya ilikuwa ni:
1) Ukuaji mkubwa wa shughuli za kiuchumi
huko Ulaya baada mapinduzi ya kiviwanda
2) Mageuzi ya kijamii na kisiasa
yaliyofungamana na mabadiliko ya kiuchumi
3)
Ugunduzi wa teknolojia ya upigaji chapa
17
Mpaka sasa hakuna vigezo maalumu vya
uainishaji wa riwaya, kila mtaalamu huangalia kwa jinsi anavyoona yeye. Wengine
wanaangalia muundo, mtindo, umbo, lengo/shabaha/historia. Madumula (2009:61 anasema
“riwaya inaweza kuainishwa kifani, kidhamira, kihistoria na kiitikadi
Naye
Mulokozi M.M (1996) anaonyesha michepuo miwili ya riwaya:
1) Riwaya ya dhati
2)
Riwaya pendwa
Katika
mhadhara huu tutaangalia riwaya kama alivyoainisha Madumula
v Inahusu maisha ya mtu binafsi, yaani
mwandishi mwenyewe, tatizo hapa ni uaminifu wa mwandishi, si rahisi kuandika
kweli yote.
v Mfano katika Kiswahili ni Riwaya “Maisha
yangu baada ya miaka 50” ya Shaaban Robert
v Inahusu mtu mwingine na siyo mwandishi
mwenyewe
v Pia inahusu maisha ya mtu binafsi lakini
ni maisha ya mtu mwingine na siyo ya mwandishi mwenyewe
v Ni matukio ya kusisimua ambayo
hayajawatokea watu wengine
v Lengo kuu ni kueleza ugumu wa maisha ya
maisha ya mhusika mkuu jinsi anavyopambana na maisha. Mfano Wasifu wa
Siti Binti Saadi ya Shaaban Robert
v Ina lengo la kufundisha maadili mema
ambayo ndiyo msingi katika maisha
v Inahusu: mateso na uvumilivu, majuto
baada ya kutambua kosa. Mfano katia Kiswahili ni Adili na Nduguze,
Kusadikika, Kufikirika-zote za Shaaban Robert
v Huchanganya historia halisi na sanaa ili
kuleta maudhui Fulani
v Hazielezi matukio yote ya kihistoria
bali yale ya muhimu tu, yaliyoathiri mwelekeo na mwenendo wa jamii Fulani
v Maudhui yake ni kumbukumbu ya mambo
yaliyopita na dhamira zake huwagusa watu wengi. Mfano katika Kiswahili ni
Riwaya ya Uhuru wa Watumwa ya J. Botela, Kwa Heri Iselamagazi ya J
Mapalala, Zawadi ya Ushindi ya Beni Mtobwa, na Njozi iliyopotea ya Mung’ong’o
v Inahusu maisha ya watu na msisitizo wake
ni katika mila, desturi na mabadiliko ya kijamii
v Dhamira huanzia ngazi ya familia hadi
kitaifa na hata kiulimwengu
v Husawiri matatizo yaliyo katika jamii
kwa kuonyesha chanzo chake. Mfano katika Kiswahili ni Dunia Uwanja wa
Fujo ya Kezilahabi, Siku ya Watenzi Wote ya Shaaban Robert na Harusi ya
J.Safari
v Aina hii inaweka mkazo juu ya mikinzano
ya ndani ya binadamu, kiakili, kinafsi na kijinsia
v Huonyesha uwezo na udhaifu wa binadamu
katika kuzikabili hali ngumu za maisha
19
v Mhusika mkuu husukumwa katika ukingo wa
aidha kufa ili ayaepuke matatizo au aishi na hayo matatizo. Mfano katika
Kiswahili ni riwaya ya KIU ya Muhamedi S.Abdalah, Nyota ya Rehema ya
huyu huyu Muhamed, Rosa Misitika ya Kezilahabi na Kichwa Maji ya
Kezilahabi
v Ni riwaya ambayo inajadili matatizo ya
kisiasa
v Inalenga kuleta mabadiliko ya kisiasa na
kijamii
v Mara nyingi riwaya za kimapinduzi zina
mwelekeo wa kisosholisti ambapo mlengwa mkuu ni umma kushika hatamu
v Mkazo upo katika ITIKADI kama msingi na
dira ya kuongoza jamii
v Wahusika wake wanatoka katika matabaka
mbalimbali
v Mfano katika Kiswahili ni riwaya ya KULI
ya Adamu Shafi, Utengano ya Saidi A Mohamed, Dunia Mti Mkavu ya S.A.Muhamedina
KASRI MWINYIFUAD ya Shafi A Shafi
v Inajadili migogoro na maisha ya binadamu
kwa kutafakari kwa mantiki na kwa kina kuhusu mambo yanayohusu maisha
v Inajadili maswali kama vile: maana ya
maisha nini? Hatima ya binadamu nini? Uhusiano wa binadamu na malaika ukoje?
v Mifano ya riwaya ya kifalsafa ni:
Mzingire, dunia uwanja wa fujo, Nagona, babu alivyokumbuka ya S.A Muhamedi,
Riwaya ya Binadamu-ya K.w Wamitila. Riwaya hizi ni ngumu sana kuelewa
zinaelezea, hata wahusika wake ni wa kufikirika zaidi, mfn wanyama nk
20
v Ni riwaya ambazo hujishughulisha na
masuala ya upelelezi, mapenzi na ujasusi, mara nyingine zinahusisha mapigano ya
kimwili na ya kiakili kati ya mtu mmoja na watu wengi. Na mara nyingi huyu mtu
mmoja huwashinda watu wengi
v Riwaya hii inakuwa na mhusika mkuu
mkweli (ambaye anapewa sifa ambazo zinazidi uwezo wa mwanadamu wa kawaida-yaani
huwezi kumshinda kuanzia mwanzo hadi mwisho). Riwaya za namna hii zina chumvi
nyingi. Mfano Riwaya ya “Kifo ni haki yangu” mhusika wake mkuu Camila anayekata
nyeti za wanaume. Mfano mwingine ni Simu ya kifa ya Faraji Katambula, Kikosi
cha Kisasi ya E.Musiba. Mzimu wa watu wa kale, Kosa la Bwana Msa-vya Muhamedi
S.Abdula-mhusika wake mkuu ni Msa
v Utanzu wa riwaya umekuja baada ya utanzu
wa ushairi na tamthiliya lakini ukuaji wake umekuwa kwa kasi kubwa. Inasemekana
kwamba riwaya ya Kiswahili ilianza kujitokeza katika mwisho mwa karne ya kumi
na tisa. Kwa nini ilichelewa sana hapa Afrika? Sababu yake ni kwamba
1.
Hadhira kubwa ya watu haikujua kusoma na kuandika
2.
Hadhira kubwa ya watu haikuweza kununua vitabu
3.
Jamii ya waswahili haikuwa na mitambo ya kupigia chapa na pia haikuwa na mfumo
mzuri wa usambazaji vitabu(hapakuwa na printers nk) 21
Hivyo tunaona kwamba wakati wa ujio wa
wakoloni ulisababisha kuanzishwa kwa baadhi ya vituo vya kupigia chapa, kwa
mujibu wa Mulokozi ( ) anasema ukoloni uliweka mazingira ambayo yameweza kuilea
riwaya. Mfano: hati ya maandishi ya Kirumi, mfumo wa usambaji wa vitabu
Mwanzo
riwaya ya Kiswahili ilianza kujitokeza kwanza kama tafsiri ya kazi za nje,
hivyo tafsiri nayo ilisaidia sana kuchipuka kwa riwaya. Kwa kadri tafsiri
zilivyokuwa zikifanywa, waswahili walianza kuiga vitabu hivyo.
Kamati
hii ilihimiza uandishi katika lugha ya Kiswahili kwa njia ya kushindana. Hivyo
ilianzisha mashindano ya uandishi wa Kiswahili. Riwaya ya kwanza ya Kiswahili
ilikuwa Uhuru wa Watumwa ya MBOTELA Ilichapwa mwaka 1934, riwaya nyingine ni
riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale”na “Simu ya Kifo”
Kulijitokeza
riwaya ambazo zilikuwa zikifuata mkondo wa kingano.Njogu na Chimerah (2008)
wanaeleza kuwa”kimaudhui riwaya nyingi zilikuwa na mambo ya kimila na tabia
kama njia ya kutunza maadili. Miongoni mwa riwaya hizo ni Utu bora mkulima,
Kufikirika, Kusaidikika, Adili na Nduguze na Siku za watenzi wote zote za
Shaaban Roberti.
Kulikuwa
na mambo yafuatayo:
Ukombozi
wa bara la Afrika na ujenzi wa jamii mpya, hivyo maudhui yake yalikuwa ni
ujenzi wa jamii mpya na: 22
• Kusuta ubinafsi na ukandamizaji
•
Zilikuwa zikihakiki unyama wa maisha ya kimiji
•
Zilikuwa zikiielekeza jamii katika mkondo wa kibinadamu katika usawa na ustawi.
Mfano riwaya hizo ni LILA NA FILA, KABURI BILA MSALABA-iliandikwa na
KAREITHI
Katika
kipindi hiki pia kulijitokeza kundi la Riwaya Pendwa zilizohusu upelelezi na
uharifu mfano Mzimu wa watu wa kale, Kisima cha Giningi, Simu ya Kifo
Zile
za uharifu ni MTAKA YOTE HUKOSA YOTE ya Leo Odera Omera, Tatizo Kisauni ya
CHADHORO
v Ni kipindi cha kupevuka na kushamiri kwa
riwaya ya Kiswahili, katika kipindi hiki riwaya nyingi zilianza kujishughulisha
na uongozi na usaliti wa kisiasa.
v Njogu na Chimerah (2008) wanadai wasanii
walianza kutafakari jinsi ukoloni ulivyoanza kufungua milango kwa watu wachache
na kutumia mali kwa manufaa yao wenyewe
v Katika kipindi hiki kuliibuka riwaya za
kihistoria kwa mfano KWA HERI ISELAMAGAZI iliyoandikwa na Mapalala. Miradi Babu
ya wazalendo.
v Katika kipindi hiki kulizuka riwaya ya
kifalsafa na ya majaribio. Mfano Nagona 1987, Mzingile(1991)-Kezilahabi. Riwaya
ya Zilahiri na Zirani ya William
v Katika kipindi hiki kulikuwa na ongezeko
la riwaya ya vijana na watoto. Mfano wa riwaya hizo ni Mashujaa wa Kaza
kamba-ya Shija (1980) wimbo wa Sokomoko (1990), Ngome ya Mianzi (1990), Ngoma
ya
23
Mianzi(1991)
Moto wa Mianzi (1995) zote hizi ni za Mulokozi.
Fasihi
huithamini jamii kihistoria, kiitikadi, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na
kijamii, na kwa kuwa jamii imekuwa ikibadilika badilika kimtazamo, fasihi nayo
imekuwa ikibadilika kwa sababu jamii inabadilia. Na hivyo fasihi nayo inahitaji
kupokea mabadiliko hayo ili kwendana na jamii husika.
Mabadiliko
katika riwaya (fasihi) yanatokea kwa sababu ya wasanii kutumia vionjo vipya
katika kuziumba kazi zao. Kama anavyosema Khamisi (2007) anasema,mara moja
tunaona neno kionjo linajisemea lenyewe kimya kimya juu ya mabadiliko ya utanzu
wa fasihi. Lengo la mabadiliko hayo ni kwamba “chenye mwanzo hakikosi kuwa na
mwisho”
Utanzu
wa riwaya ya Kiswahili haukuepuka mabadiliko. Sababu zilizobadilisha mabadiliko
haya ni makali ya wembe wa kisiasa, mfano nchini Kenya makali ya kisiasa
yalikuwa dhidi ya Masosholisti. Mfano wa riwaya ni Gamba la Nyoka,
Majaribio
na mabadiliko ya riwaya ya Kiswahili yalianza pale ambapo waandishi wengi wa
Kenya na Tanzania walipoanza kukataa kukubali kila kitu walichokisikia. Walipoanzaa
kukataa kanuni za jamii za ughunaji, hivyo wakaanza kuandika riwaya tofauti na
za mwanzo. 24
Madumula
anawanukuu SCHOLES na APLLOE riwaya huweza kubadiliko kutokana na utanzu
wenyewe kuwa hauna mashiko legelege na tepetepe, hubadilika badilika
Hivyo
kutokana na majaribio na mabadiliko katika riwaya ya Kiswahili tunaona upywa
katika kazi za riwaya katika fani na maudhui yake. Kisanaa riwaya hizi
zinachanganya uhalisia na falsafia. Mfano wa riwaya ya Kufikirika. Mfano
mwingine ni UKIUSHI-Mtiririko haueleweki, na riwaya hizi zinakuwa na
mwingiliano matini yaani kuchanganya kazi nyingi katika kazi moja.kisanaa pia
zina wahusika wa kidhani
Pia
riwaya hizi zina mazingaombwe sana, kwa mfano katika Nagona lugha yake ni ya
mafumbo, visasili, pia ni lugha inayoelekeza, haifafanui sana.kimaudhui riwaya
hizi za majaribio inatazama matatizo kwa mtazamo wa ndani. Inashughulikia
masuala ya ulimwengu wote, riwaya hizi pia kimaudhui zinaitetea dunia dhidi ya
maangamizi ya uovu mkubwa.
3.
TAMTHILIYA NA DRAMA
Kumekuwa
na mkanganyiko kati ya dhana hizi mbili, watu wamekuwa wakizichanganya sana.
Tamthiliya ni drama na kinyume chake
Tamthiliya ni drama lakini si drama zote ni tamthiliya
A. TAMTHILIYA
Mulokozi (1999:88) tamthiliya ni kazi iliyokusudiwa kutendwa jukwaani kwa ajili
ya hadhira fulani
25
Tamthiliya huitwa mchezo wa kuigiza. Istilahi hii tamthiliya imetokana na neno
methali lenye maana ya mfano/ishara ya kitu
Wamitila (2003)tamthiliya ni kazi ya kidrama na ya kimaongezi ambayo huigizwa
mbele ya hadhira/kazi iliyoandikwa ili kusomwa
Kimuundo tamthiliya hudhihilika katika:
matendo
na maonyesho, mazungumzo huchukua sehemu kubwa katika uwasilishwaji wake wa
maudhui (huwa katika diolojia)
haiweki
msisitizo mkubwa katika uwasilishwaji wake jukwaani wakati drama inaweka
msisitizo mkubwa katika uwasilishwaji wake
Penina
Mhando anadai kuwa “Tamthiliya ni ule utungo unaoweza kuwa umeandikwa au
haukuandikwa ambao ambao unaliweka wazo linalotaka kuwasilishwa katika umbo la
tukio la kiliwezesha kutendeka mbele ya hadhira”
Kutokana na sifa hii ya kutendeka jukwaani tamthiliya inawekwa kwenye kundi la
sanaa za maonyesho(Mulokozi)
SANAA
ZA MAONYESHO
Mohamedi
na Balysidya wanasema kuwa sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa 4
a) Mchezo
b) Mchezaji
c) Uwanja wa kutendea
d)
Watazamaji
©tamthiliya
ni andiko la kiuigizaji linalotoa simulio kwa kuonyesha maneno na matendo 26
B.
DRAMA
Wamitila
(2003) anasema “ ni aina ya utanzu wa fasihi ambao kimsingi hudhamiriwa
kuigizwa mbele ya hadhira” inaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa lakini
msisitizo wake ni kuigizwa
Msingi mkuu wa drama ni utendaji na utanzu huu umebuniwa kwa ajili ya thieta
Wahusika hupewa majina ya kuigiza mbele ya hadhira
Iwochukuu
(2000) anasema “drama ni mabadiliko, ubunifu na usawiri wa uhalisi jukwaani.
Msingi mkuu wa drama ni matendo. Hoja hii imeungwa mkono na Aristotle
anayeifafanua drama kama uigaji wa matendo
Bretcht anasisitiza kuwa drama si uigaji wa matendo pekee pia ni chombo cha
ufafanuzi wa hali za kijamii, chombo cha mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi
Kitendo huitwa drama endapo kitendo hicho ni mwigo wa kitendo cha
kilichokwishatangulia.
DRAMA
ZA KIJADI
Jamii
ya waafrika ikiwemo ambayo utamaduni wake ulikuwa haujaingiliwa na wakoloni
ilikuwa na sanaa ya maonyesho zilizogawanyika katika makundi mbalimbali.
Balisdya na Mhando walianisha aina mbalimbali za drama hizo
1. SHEREHE
Zilihusishwa na kundi moja kwenda
kundi jingine mfano. Jando na unyago, jina kwa mtoto, kuota meno nk
Ziliambatana na madaraka kwa mwanajamaii ya mwanajamii aliyeingia katika kundi
jipya. sherehe
27
ziliwekwa katika katika umbo la vitendo
na vikapewa uzuri wa kisanaa
2. NGOMA
Mhando na Balisdya wanasema ni chombo,
sherehe au uchezeshaji wa viungo vya mwili. Malengo yake ni kuburudisha
3. MASIMULIZI YA HADITHI
Katika usimuliaji wa hadithi kuna
vipengele vya kidrama vinavyojitokeza. Yaani:
v Usimuliaji
v Uigizaji
v Uimbaji
v Muziki
4. KUSALIA MIUNGU
Jamii fulani inapopata mafanikio au
matatizo fulani ndipo huenda kutambikia miungu yao kwa kushukuru au kuomba
kutatuliwa matatizo yao
5. MAJIGAMBO
Masimulizi ya kujigamba ya mtu kuhusu mambo
ya kishujaa aliyopata kuyatenda maishani mwake
Kwa kawaida hutumia lugha ya kishairi
na masimulizi huambatana na vitendo vya majigambo yenyewe.
Pia yaliambatana na matumizi ya maleba
AINA
ZA TAMTHILIYA
1. TANZIA
Ni tamthiliya yenye huzuni inayogusa hisia za wasomaji kiasi cha kuogopesha na
kumuonea huruma mhusika mkuu ambaye hupatwa na masahibu/matatizo/majanga hayo
28
Msingi mkuu inalenga msomaji kupata hisia
Mhusika mkuu huwa ni maarufu
Aristotle anasema kuwa “ mhusika mkuu lazima atoke katika familia yenye nasaba
bora/tabaka la juu”
Si tanzia zote mhusika anatoka tabaka la juu. Mfano KIFO KISIMANI-mhusika mkuu
hapa anatokea katika tabaka la chini kabisa
Misingi
ya utokeaji wa tanzia
Iamushe hisia za woga na huruma miongoni mwa hadhira
Shujaa lazima awe mtu mwema, sura nzuri,umbo zuri, ili yanayomtokea
yasitarajiwe
Mhusika huonyesha kuumia kadri mtu anavyoonekana kuwa ni mwema na ana umbo
zuri.
Anguko la shujaa huja kutokana na uamuzi wake ama kosa lake mwenyewe
Katika tanzia ya kirasimi shujaa hutoka katika nasaba bora
2.
RAMSA/KOMEDI
Ni tamthiliya ambayo inachangamsha na huishia kwa kufurahisha/ni tamthiliya ya
vichekesho, hii haina maana kwamba haina maudhui mazito ndani yake.
Inashughulikia mambo yale yale yanayoweza kushughulikiwa na tanzia. Mfano
masuala ya unafiki,uzembe, wivu nk, hata hivyo inayashughulikia kwa namna
tofauti na tanzia
Kwa kawaida wahusika wa Ramsa huumbwa vibaya kuliko walivyo
Udhati wa ramsa si kwamba usanii humalizika katika kicheko/furaha zaidi ni
kuishia mhusika mkuu kufanikiwa
shujaa
wa kiramsa 29
Si lazima awe
mtu maalum/mbabe au shujaa, anaweza kuwa mtu wa kawaida
Kwa mujibu wa Aristotle anasema mhusika wa ramsa lazima awe mtu wa wastani
chini ya wastani, awe ni mtu ambaye hatarajiwi kujitokeza na mtu wa nasaba duni
na matendo yake yawe ya ucheshi
Ni lazima awe mtu ambaye akifanikiwa wasomaji au watazamaji watafurahi
uhusika
wa wahusika wa ramsa
Ramsa inawahusu watu wa kawaida kuliko ilivyo tanzia
Inawahusu watu wa kipato cha kati na cha chini
Na dhamira zote huelekezwa kwa watu wa kipato cha chini na duni. Mfano
walalahoi
AINA
ZA RAMSA
a) UTANI
Ni aina ya ramsa ambayo mambo
inayozungumzia yanaokana kuwa ya kipuuzi
Mambo hugeuzwa kuwa kinyume kabisa na
jinsi yalivyo
Kwa kawaida sura za wahusika
hubadilishwa kuwa kama vinyago
Lengo kuu ni kuchekesha-ambalo ndilo haswaa, lengo la tamthiliya ya ramsa
b)
RAMSA ZA MAPENZI/MAHABA
30
Hizi zinahusu mapenzi ambapo wapendanao huwekewa vikwazo kama vile fedha,
elimu, din, kabila nk
Wahusika hawa hushinda vikwazo hivyo
c)
TASHTITI/DHIHAKA
Zinalenga kwa viongozi wa kisiasa au dini
Zinawahusu matapeli, wanafiki, wala rushwa, ni
Mhusika mkuu anakuwa na sifa za utapeli nk
Lengo kuu ni kumdhihaki huyu kiongozi ili aachane na tabia hizo
ni njia ya walalahoi kupeleka malalamiko yao kwa viongozi
SIFA
ZA RAMSA
Sharti ivutie akili na siyo hisia
Ni lazima kuwa na matendo bila kufikiria hii itapelekea msomaji au mtazamaji
kujua kwamba wahusika hawa hawana akili
lazima iwe na hali ya utu (ikitukumbusha ubinadamu wetu)
sharti iwe na mila na desturi ambazo hadhira inazifahamu toka katika jamii yake
Hadhira isiogope au kupata uchungu kwa sababu hii sio lengo lengo la ramsa
Wahusika wa ramsa hujaribu kuepuka vikwazo ambavyo vimewekwa
Inaonyesha haja ya kuikomboa nafsi
Mfano
wa ramsa ni kama vile MFALME JUHA
d)
TANZIA-RAMSA
31
Hii ni tamthiliya ambayo inaonyesha mabaliko ya aina fulani yanayogeuza matukio
ya tanzia kuwa ya ramsa
Ni tamthiliya inayochanganya vipengele vya tanzia na ramsa
Hutumiwa sawa na tamthiliya ya kibwege-hii ni tamthiliya
ambayo inaonyesha kwamba kicheko au furaha ndiyo jibu pekee la maisha kwa watu
ambao hawana imani na maisha ambao kwao misingi dhabiti ya maisha imeondoleo.
Mfano tamthiliya ya AMEZIDI ya S.A Mohamedi
e)
MELO-DRAMA
CHIMBUKO
, MABADILIKO NA MAENDELEO YA TAMTHILIYA YA KISWAHILI
CHIMBUKO:
Tamthiliya
chimbuko lake duniani kote linashahibiana/zinapatikana duniani kote na
kuonekana katika maumbo tofauti tofauti. Tamthiliya inahusishwa sana na
visakale na matendo ya kidini. Katika bara la Ulaya tamthiliya inahusishwa na
miviga ya kidini katika jamii ya Wayunani/Wagiriki wa zamani/ancient Greek.
Miviga hii katika jamii ya wayunani iliambatana na dua ya kuzaliwa..mpaka kufa
na kuoza na kuwa binadamu tena
Huko
India tamthiliya
zilitokana na tenzi zilizoitwa Mahabharata na ………pia zilitokana na
miviga zilizoendana na utendi wa tendi hizo kutika mahekalu ya kidini
Kule
Japani na China-drama
inatokana na dansi na miviga ya kidini baadaye miviga hii ilijitenga na dini na
kuanza kujishughulisha na sanaa
Katika
Afrika-maigizo
ya tamthiliya yalikuwa yanapatikana huko Misiri na maigizo haya yalikuwa 32
yanahusu kufa na kufufuka kwa mungu wa
wamisiri aliyeitwa osiais. Miviga hii ilikuwa inaigizwa kila mwaka kwa
miaka kama elfu mbili. Pia katika Afrika kulikuwa na maigizo ambayo hayakuwa
yameandikwa lakini yalikuwa ni sehemu ya matendo ya kijamii yaani miviga na
ngoma. Kulikuwa na tamthiliya bubu, maigizo ya watoto na maigizo ya watani.
Drama hizi zilikuwa zikifungamanishwa na fasihi simulizi
Hivyo
tamthiliya inatokana na mambo makuu matatu
a. Miviga na viviga vya kijamii, na dini
pamoja na tendi
b. Usawilishaji wa maisha ya kawaida kwa
ajili ya burudani, elimu nk
c.
Sanaa za maonyesho za kijadi; ngoma na dansi
marejeo hamuna ,ula asnt sana
ReplyDelete